Pata taarifa kuu
AU-UCHUMI

Mawaziri wa fedha na utengamano kutoka Afrika wakutana Yaounde

Mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, ambako kunafanyika mkutano wa mawaziri wa fedha na utangamano wa kikanda kutoka nchi wanachama za Umoja wa Afrika.  (Picha ya kumbukumbu)
Mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, ambako kunafanyika mkutano wa mawaziri wa fedha na utangamano wa kikanda kutoka nchi wanachama za Umoja wa Afrika. (Picha ya kumbukumbu) Tim E. White/Getty Images

Mkutano wa mawaziri wa fedha na utangamano wa kikanda kutoka nchi wanachama za Umoja wa Afrika unang’oa nanga hivi leo jijini Yaounde, Cameroon wakati huu nchi wanachama zikizidisha kasi katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa bara hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ambao ni watatu kufanyika, unawakutanisha mawaziri kutoka kwenye nchi wanachama za Umoja wa Afrika, wakurugenzi wa taasisi za kifedha, wadau kutoka sekta binafsi na vyombo vya habari.

Mawaziri hawa pamoja na wataalamu mbalimbali wa masuala ya fedha, uchumi na mipango, watajadiliana kuhusu namna bora ya kuhuisha sera za nchi wanachama kwaajili ya kuongeza uzalishaji wenye tija kwa bara la Afrika.

Mbali na kujadili masuala ya kisera, mawaziri hawa pia, wataangazia kwa kina mchango wa utangamano wa kikanda na sekta binafsi katika kuongeza uzalishaji ili kutengeneza soko lenye ushindani kwa bidhaa kutoka barani Afrika.

Wataalamu wanasema kuwa licha ya uchumi wa bara la Afrika kuimarika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, bara hili bado linakabiliwa na hali duni ya uzalishaji kwa kutegemea kuuza bidhaa zisizokuwa na thamani hali ambayo haitoi majibu kwa tatizo la ajira na mapambano dhidi ya umasikini.

Katika ripoti yake ya mwaka jana kuhusu maendeleo ya bara hilo, Umoja wa Afrika ulisema licha ya kuwa bara hili lina utajiri mkubwa wa rasilimali kama vile, mafuta, gesi na madini, bado linaorodheshwa kuwa miongoni mwa kanda masikini.

Hivi karibuni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake rais wa Rwanda Paul Kagame, aliwataka viongozi wenzake kuongeza kasi ya utekelezaji wa itifaki mbalimbali walizoridhia, huku akisisitiza nchi wanachama kutoa kipaumbele katika matumizi ya TEHAMA akisisitiza ndio njia pekee ya kulikwamua bara la Afrika kimaendeleo.

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Sera bora kwa uzalishaji wenye tija”.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.