Pata taarifa kuu
ANGOLA-DOS SANTOS-UCHUMI-HAKI

Angola: Mali Za Binti ya Rais wa zamani Dos Santos zazuiliwa

Mfanyabiashara Sindika Dokolo pamoja na mkewe, Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa Angola.
Mfanyabiashara Sindika Dokolo pamoja na mkewe, Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa Angola. © AFP PHOTO/ PUBLICO/ FERNANDO VELUDO

Binti ya Rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos, Isabel dos Santos pamoja na mumewe Sindika Dokolo, wanaendelea kukabiliwa na mkono wa sheria nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Mkoa wa Luanda imechukua uamuzi wa kuzuia kwa muda akaunti za benki na hisa za binti na mkwe wa rais wa zamani wa nchi hiyo José Eduardo dos Santos.

Isabel dos Santos na mumewe Sindika Dokolo, wanahisa katika benki kadhaa na makampuni kadhaa, wanashtumiwa kwamba walinunua hisa na pesa za kampuni ya mafuta ya umma ya Sonangol. Binti mkubwa wa rais wa zamani wa Angola, anayechukuliwa kama mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo ya mafuta ya umma hadi mwezi Novemba 2017.

Mwanaharakati wa kupambana na ufisadi Rafael Marques ametaja, kwa mfano, kununuliwa kwa udanganyifu hisa kutoka kwa kampuni ya simu Unitel, au kutoka kwa kampuni ya mafuta ya Ureno Galp.

Katika taarifa ya mwendesha mashtaka wa umma, serikali ya Angola pia imetangaza kwamba imefanyiwa dhulma ya zaidi ya dola bilioni moja. Sababu: mkopo uliochukuliwa kwa dhamana haujalipwa.

Mfanyabiashara mwingine na mmoja wa washirika wao, Mario Filipe Moreira Leite da Silva, pia amejikuta mali zake zimezuiliwa kwa muda na mahakama.

Rais mpya Joao Lourenço, aliyechaguliwa mnamo mwaka 2017, ameapa kupambana dhidi ya ufisadi.

Isabel dos Santos si mtu wa kwanza kutoka familia ya mtangulizi wake José Eduardo dos Santos kushtakiwa.

Mtoto wake wa kiume José Filimino Dos Santos, mkuu wa zamani wa Mfuko wa uwekezaji wa Angola, ameendelea kufikishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Luanda tangu Desemba 9 kwa ufisadi na utakatishaji fedha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.