Pata taarifa kuu
Norway

Anders Breivik ahukumiwa miaka 21 kwa mauaji nchini Norway

REUTERS/Heiko Junge

Mahakama ya jijini Oslo nchini Norway hii leo imemhukumu kifungo cha miaka 21 gerezani kijana aliyetekeleza mauaji ya watu 77 , Anders Behring Breivik tukio ambalo liliishitua nchi hiyo Mwaka jana 

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imemkuta na hatia Breivik kwa kujihusisha na vitendo vilivyoelezwa kuwa vya kigaidi vilivyotokea tarehe 22 mwezi julai mwaka jana vilivyohusisha shambulio la Bomu la jijini Oslo.

Shambulio lilisababisha watu wanane kupoteza maisha halikadhalika shambulio la risasi lilitekelezwa katika kisiwa cha Utoia na kugharimu maisha ya watu 69 wengi wao Vijana waliopiga kambi kisiwani humo.

Awali Breivik a.isema kuwa hata kata rufaa dhidi ya kiungo cha gerezani alipokuwa akipinga taarifa kuwa alikuwa amerukwa na akili wakati alipokuwa akitekeleza mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa Sheria za Norway nchi hiyo haina hukumu ya kunyongwa wala kifungo cha maisha hata hivyo kwa wafungwa waliomaliza adhabu zao huendelea kushikiliwa ikiwa bado wataendelea kuwa tishio katika jamii.

Breivik mwenye miaka 33 alikiri kutekeleza mashambulizi akijiona kuwa shujaa katika kile alichokiamini kuwa vita dhidi ya uislamu na wale wote wanaounga mkono tamaduni mbalimbali za kigeni nchini humo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.