Pata taarifa kuu
UKRAINE-VITA-USALAMA-SIASA

Machafuko yazuka upya Mashariki mwa Ukraine

Wanajeshi wa Ukraine katika mji wa Horlivka, kaskazini mwa Donetsk, mashariki mwa Ukraine, Juni 6 mwaka 2015.
Wanajeshi wa Ukraine katika mji wa Horlivka, kaskazini mwa Donetsk, mashariki mwa Ukraine, Juni 6 mwaka 2015. Reuters/Oleksandr Klymenko

Eneo la Mashariki mwa Ukraine limeendelea kukabiliwa na machafuko na visa vya mauaji katika siku za hivi karibuni kufuatia vita kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo hilo, ambao wanaungwa mkono na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano yamesababisha vifo vya watu 6,500 tangu mwezi Aprili mwaka 2014.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI nchini Mosco, Veronika Dorman, masaa 48 yaliyopita yamekuwa hasa yenye vurugu mashariki mwa Ukraine. Duru kutoka eneo hilo zinafahamiswa kwamba mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu wengi ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida na wanajeshi, huku watu wengi wakijeruhiwa. Mapigano yameshika kasi pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Donetsk.

Mashambulizi ya mabomu yameongezeka katika mji huo wa Donetsk, Mashambulizi hayo yameathiri maeneo ya makazi, na kuharibu majengo ikiwa ni pamoja na hospitali na kusababisha ajali mbalimbali hasa majengo kadhaa yaliteketezwa kwa moto. Waasi na jeshi la Ukraine wamekua wakilaumiana kila upande kuuhusisha mwengine na mashambulizi hayo. Hii ni mara ya kwanza jiji la Donetsk linalengwa na mashambulizi tangu kuafikiwa mkataba wa kusitisha mapigano mwezi Februari mwaka 2015.

Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la Mashariki mwa Ukraine, ambao wanaungwa mkono na Urusi pamoja na wanajeshi wamekua wakinyoosheana mara kwa mara kidole cha lawama kwa kutumia silaha kubwa za kivita, na kukiuka makubaliano ya Minsk ambayo yanaeleza kuondolewa kwa silaha kubwa za kivita kwenye mstari wa mbele wa vita. Zoezi la kuondoa silaha hizo, kwa mujibu wa waangalizi wa OSCE, na mashahidi wengi kwenye uwanja wa vita, lilikua bado kukamilika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.