Pata taarifa kuu
ULAYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Ulaya yakabiliwa na ongezeko la wahamiaji

Wakimbizi wakijiandaa kuingi katika trenikwa kuelekea Munich katika kituo cha treni cha Vienna, Septemba 1, 2015.
Wakimbizi wakijiandaa kuingi katika trenikwa kuelekea Munich katika kituo cha treni cha Vienna, Septemba 1, 2015. REUTERS/Leonhard Foeger

Mamia ya wahamiaji wanaoshinikiza kusafiri kwenda nchini Ujerumani wamekabiliana na polisi wakutuliza ghasia nchini Hungury, wakati huu takwimu mpya zikionesha kuwa idadi ya wakimbizi wanaoingia barani Ulaya inazidi kuongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na wahamiaji IOM, linasema kuwa zaidi ya wahamiaji laki 3 na elfu 50 wengi wakitokea nchini Syria, wamehatarisha maisha yao kwa kusafiri kupitia bahari ya Mediterania.

Jumatatu wiki hii mamia ya wahamiaji walikusanyika kwenye kituo kimoja cha Treni za abiria mjini Budapest, wakishinikiza vyombo vya usalama kuwapakia na kuwasafirisha kwenda nchini Ujerumani, lakini wakakutana na upinzani kutoka kwa polisi.

Nchi ya Hungury inasema kuwa inatumia na kufuata sheria za Umoja wa Ulaya kwa kuendelea kuwazuia wahamiaji hao kuingia nchini mwao na kwenda kuomba hifadhi Ujerumani na nchi nyingine za ulaya, hatua ambayo inakisolewa na baadhi ya mataifa.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hali hii isipodhibitiwa na viongozi wa ulaya kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na wimbi hili la wahamiaji, huenda nchi za Ulaya zikashuhudia idadi kubwa zaidi ya wahamiaji wanaotaka hifadhi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.