Pata taarifa kuu
HUNGARY-SERBIA-WAKIMBIZI-USALAMA

Mvutano kwenye mpaka wa Hungary, wahamiaji wavunja uzio

Wahamiaji wavunja sehemu ya uzio kwenye mpaka wa Serbia na Haungary, Septemba 16.
Wahamiaji wavunja sehemu ya uzio kwenye mpaka wa Serbia na Haungary, Septemba 16. REUTERS/Marko Djurica

Wahamiaji wamefaulu kuvunja uzio kwenye mpaka wa Serbia na Croatia katika mji wa Röszkena hivyo kufaanikia kupata njia. Hungary ilifunga mpaka wake na Serbia, Jumatatu, Septemba 14.

Matangazo ya kibiashara

Tangu wakati huo, maelfu ya wahamiaji wamekusanyika nyuma ya uzio uliyojengwa kwa nyaya za chuma. Hali ya wasiwasi imeibuka kufuatia uamzi huo wa wahamiaji kujitafutia njia kwa nguvu.

Magari matatu ya kijeshi yameiwasili Jumatano kwenye mpaka kati ya Hungary na Serbia, ambako mapigano yalitokea kati ya wahamiaji na polisi ya Hungary. Wahamiaji kadhaa wamfaulu, baada ya zaidi ya saa moja ya makabiliano mapema Jumatano jioni wiki hii, huku kikosi cha kuzima fujo cha Hungary kikizidiwa nguvu na wingi wa wahamiaji, ambapo wahamiaji walipenya katika na kuingia katika ardhi ya Hungary wakitokea Serbia, wakipitia kwenye mpaka wa Röszke.

Wahamiaji wameweza kuvunja vizuizi viliyokua vimewekwa katika barabarainayoelekea Hungary. Kikosi cha ktuliza ghasia kiliamua kurudi nyuma kwenye umbali wa mita hamsini baada ya kushambuliwa na wahamiaji hao. Lakini muda mfupi baadaye kikosi hicho kijibu kwa kurusha mabomu ya machozi dhidi ya wahamiaji.

Upande wa Serbia, Sami Boukhelifa mwandishi wetu katika mji wa Horgos umeshuhudia kwamba ni vijana hasa wanaosafiri wakiwa peke yao au katika makundi ambao wameweza kuvuka mpaka licha vizuizi vya Chuma viliyowekwa na viongozi wa Budapest. Vizuizi vya nyaya za chuma, kikosi cha kutuliza ghasia, havikuwazuia wahamiaji kuendelea na harakati zao. Mizinga ya kurusha maji na mabomu ya machozi vimetumiwa dhidi ya wahamiaji waliokuwa wakijaribu kuvuka mpaka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.