Pata taarifa kuu
CROATIA-WAKIMBIZI-USALAMA

Croatia yafunga sehemu moja ya mipaka yake

Wahamiaji na wakimbizi wakiingia katika treni katika kituo cha treni cha Ilaca, Septemba 17, 2015 nchini Croatia, karibu na mpaka na Serbia.
Wahamiaji na wakimbizi wakiingia katika treni katika kituo cha treni cha Ilaca, Septemba 17, 2015 nchini Croatia, karibu na mpaka na Serbia. ELVIS BARUKCIC/AFP

Maelfu ya wahamiaji wameendelea kuingia Alhamisi hii nchini Croatia, ambapo viongozi wa nchi hiyo wanasema wamezidiwa na wameamua kufunga "hadi itakapotangazwa tena" mipaka saba kati ya nane inayopeana na Serbia.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wahamiaji 11,000 wameingia katika ardhi ya Croatia wakipitia Serbia tangu Jumatano asubuhi, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Alhamisi jioni wiki hii.

Wakati wa mchana, wizara hiyo imesema inatarajia kupokea watu zaidi ya 20,000 katika wiki mbili zijazo na wanaogopa kuwa wahamiaji huenda wakaingia kwa wingi na "kushindwa kuwadhibiti ".

Madhara ya haraka: Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kufungwa "hadi itakapotangazwa tena" mipaka ya Tovarnik, Ilok, Ilok 2, Principovac, Principovac 2, Batina na Erdut.

Uamuzi huu unashikilia shinikizo kwa Umoja wa Ulaya, ambao viongozi wake wanakutana wiki ijayo kujaribu kuweka kando tofauti zao ili kukabiliana na mgogoro huu.

Croatia ni njia mpya ya kuelekea Ulaya Magharibi baada ya kuufunga mpaka wa Serbia na Hungary, ambapo Jumatano wiki hii kulishuhudiwa makabiliano kati ya wahamiaji wenye hasira na vikosi vya usalama.

Wahamiaji walibadili njia na kuelekea Slovenia, ambapo wahamiaji 150 wameweza kuingia katika treni usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, baada ya kutishiwa kufukuzwa hadi Zagreb.

Kusini zaidi, Alhamisi asubuhi wiki hii, kituo ndogo cha treni cha Tovarnik, mji wa Croatia karibu na mpaka wa Serbia, na vitongoji vyake walivamia na wahamiaji waliokua wakitafuta kuingia katika treni ili kuelekea Zagreb na kuendelea na safari yao.

" Hapa kuna kati ya watu 4,000 na 5,000. Treni zimewasili lakini haziawezi kuchukua watu wote hawa," amehakikisha msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Jan Kapic.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.