Pata taarifa kuu
SERBIA-LIBYA-USALAMA

Maafisa wawili wa Ubalozi wa Serbia watekwa nyara Libya

ituo cha polisi jijini Tripoli kikilengwa na shambulizi la kundi la IS, Alhamisi Machi 12, 2015, Libya..
ituo cha polisi jijini Tripoli kikilengwa na shambulizi la kundi la IS, Alhamisi Machi 12, 2015, Libya.. REUTERS/Hani Amara

Maafisa wawili wa ubalozi Serbia nchini Libya, ikiwa ni pamoja na mwanamke, wametekwa nyara Jumapili hii asubuhi, wizara ya mambo ya nje ya Serbia imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

" Maafisa wawili wa Ubalozi Serbia nchini Libya wametekwa nyara Jumapili hii asubuhi", wizara ya mamabo ya nje imesema, bila hata hivyo kutoa maelezo kuhusu watekaji nyara.

Chanzo cha Wizara ya mambo ya nje ya Serbia, kimesema kuwa maafisa wawili wametekwa nyara katika mji wa mwambao wa Sabratha, ngome ya makundi ya waislamu wenye msimamo mkali, karibu kilomita 70 magharibi mwa mji mkuu wa Tripoli.

Kwa mujibu wa Belgrade, maafisa wawili waliotekwa nyara ni Sladjana Stankovic, mwanamke, anaye husika na mawasiliano, na dereva wake, Jovica Stepic.

Wizara ya mambo ya nje ya Serbia imeeleza kuwa imewafahamisha viongozi wa Libya kuhusu jinsi hali inavyoendelea na kuhakikisha kuwa itafanya kinachowezekana, licha ya hali mbaya katika eneo hilo, ili watu wake waachiliwe huru.

Akizungumza kwa kwenye runinga ya taifa (RTS), Waziri wa mambo ya nje wa Serbia, Ivica Dacic, amesema msafara wa magari ya ujumbe wa ubalozi wa Serbiaulikua njiani kuelekea Tunisia. Balozi wa Sebia alikuwa katika gari moja na watu waliotekwa nyara walikua katika gari nyingine.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.