Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Hollande ataka marekebisho ya Katiba

François Hollande mbele ya Bungeakiwahutubia wananchi jijini Versailles Novemba 16, 2015.
François Hollande mbele ya Bungeakiwahutubia wananchi jijini Versailles Novemba 16, 2015. REUTERS/Philippe Wojazer

Siku tatu baada ya mashambulizi ya kigaidi jijini Paris yaliosababisha vifo vya watu wengi, Rais wa Ufaransa François Hollande amewahutubia wananchi kupitia bunge Jumatatu jioni katika mji wa Versailles.

Matangazo ya kibiashara

"Jamhuri yetu sio makaazi ya wauaji waliodharauliwa", François Hollande amesema, ambaye amebaini "demokrasia yetu imeshinda na imepevuka kwa kweli kuliko hawa wauaji wasioeleweka."

Kwa mujibu wa Rais Hollande, Ufaransa haishiriki katika "vita vya ustaarabu". Itachukua "muda" na "subira" lakini "adui haiko mbali kufikia malengo yake."

Wahanga ni kutoka mataifa 19

Rais Wa Ufaransa ametangaza kuwa watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa katika mashambulizi yaliotokea jijini Paris na katika eneo la Saint-Denis ni kutoka "mataifa 19"

Hali ya Hatari yatazamiwa kuongezwa muda

Bunge litaombwa "Jumatano" wiki hii kupitisha muswada "unaoongeza muda wa miezi mitatu kwa hali ya hatari" na "kurekebisha maudhui yake kwa maendeleo ya teknolojia na vitisho."

Mashambulizi yatajwa kuwa vita dhidi ya Ufaransa

"Vitendo vya vita vilitangazwa Ijumaa wiki iliopita, viilipangwa nchini Syria, viliandaliwa Ubelgiji, na kutekelezwa katika ardhi yetu ya Ufaransa kwa ushirikiano na baadhi ya raia wa Ufaransa", Rais François Hollande amesema.

Hollande alinyooshea kidole cha lawama IS

Rais wa Syria Bashar Al Assad "hawezi kuwa pingamizi lakini adui yetu nchini Syria ni kundi la IS". Hollande anataka "kuzuia" kundi la Islamic State (IS) "kutumia wapiganaji wa kigeni kili kutekeleza mauaji katika mipango yao iliopangwa kutoka Syria na Iraq."

Hollande atoa wito wa kukutana kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Rais wa Ufaransa ameomba mkutano wa Baraza la Usalama "haraka iwezekanavyo kupitisha azimio kuashiria nia hii ya pamoja ya mapambano dhidi ya ugaidi", akihakikisha kuwa "haja ya kulitokomeza kundi la IS ni suala ambalo linahusu jumuiya ya kimataifa. "

Rais Hollande ahadi kukutana na Obama pamoja na Putin

"Nitakutana katika siku zijazo na Rais Obama na Rais Putin kwa kuunganisha majeshi yetu na kufikia matokeo ambayo kwa sasa bado hayajatangazwa", amesema. "Ufaransa inaongea na wote, Iran, Uturuki, nchi za Ghuba", Rais Hollande amesisitiza.

Ukaguzi kwenye mipaka

Rais Francois Hollande ameomba "kuanzishwa kwa zoezi la ukaguzi na utaratibu kwenye mipaka" ya Umoja wa Ulaya na "kibali kabla ya mwisho wa mwaka 2015" cha faili ya abiria wa Ulaya wanaosafiri kwa ndege (PNR) kwa ajili ya "kuwa na uhakika wa kurejea kwa wanajihadi na kuwakamata. "

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.