Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-MASHAMBULIZI-UGAIDI-USALAMA

Mashambulizi ya Paris : watuhumiwa 5 kati ya 7 waachiliwa huru Brussels

Operesheni ya polisi Novemba 16, 2015 katika wilaya ya Molenbeek, Ubelgiji.
Operesheni ya polisi Novemba 16, 2015 katika wilaya ya Molenbeek, Ubelgiji. AFP/AFP

Watu 5 kati ya saba waliokamatwa nchini Ubelgiji katika sehemu ya uchunguzi wa mashambulizi yaliosababisa vifo vya watu wengi mjini Paris wameachiliwa huru, ikiwa ni pamoja na Mohamed Abdeslam, ndugu wa mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga, chanzo cha mahakama jijini Brussels kimebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla watu watano wameachiwa huru" na "wawili wanaendelea kuzuiliwa kwa muda", Ofisi ya mashtaka ya Ubelgiji imeliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Mohamed Abdeslam ameachiliwa huru "bila mashitaka yoyote," mwanasheria wake aliliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Ni sahihi", amejibu msemaji wa Ofisi ya mashitaka kwa swali aliloulizwa kuhusu kama operesheni hiyo inalenga kumpata Abdeslam Salah.

Msemaji wa Ofisi ya mashitaka hakua hata hivyo nauwezo wa kusema kama mtuhumiwa, analengwa na hati ya kimataifa ya kukamatwa na kuwasilishwa kama "mtu hatari", yupo katika nyumba iliyozingirwa na polisi katika wilaya ya Molenbeek.

Chanzo kutoka Ufaransa awali kililiambia shirik ala habari la AFP kwamba "uchunguzi" umekua ukifanyika " kuhusu kuwepo kwa Salah Abdeslam katika ghorofa" ya mji huo maarufu mjini Brussels, ambayo askari polisi wengi wamepelekwa, wakiandamana na maafisa wa Zima moto na timu za kutegua Mabomu.

Abdeslam Salah ni mtuhumiwa muhimu katika uchunguzi wa mashambulizi yaliyotokea jijini Paris Ijumaa usiku wiki iliyopita.

Raia huyu Mfaransa alizaliwa jijini Brussels, na kuelezwa kama mtu "hatari" na polisi wa Ufaransa katika taarifa ya kumsaka iliyorushwa hewani Jumapili jioni na kuelezwa na vyombo vya habari vya Ubelgiji kama "adui wa umma namba moja", anatuhumiwa kuhusika katika mashambulizi pamoja na ndugu zake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.