Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-MASHAMBULIZI-UGAIDI-USALAMA

Mashambulizi ya Paris: watuhumiwa wawili kushtakiwa Ubelgiji

Vikosi vya polisi wa Ubelgiji katika wilaya Molenbeek, Novemba 16, 2018.
Vikosi vya polisi wa Ubelgiji katika wilaya Molenbeek, Novemba 16, 2018. DIRK WAEM/BELGA/AFP

Watuhumiwa wawili wameshtakiwa kwa makosa ya ugaidi Jumatatu hii jijini Brussels kufuatia mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi mjini Paris, nchini Ufransa.

Matangazo ya kibiashara

Lakini operesheni kubwa polisi ilioendesha katika wilaya ya Molenbeek imeshindwa kumkamata mtuhumiwa muhimu katika mashambulizi hayo, Salah Abdeslam, anaye lengwa na kibali cha kimataifa cha kukamatwa.

Watuhumiwa wote wawili wameshtakiwa kwa makosa ya "kigaidi" na "kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi" na wamewekwa chini ya ulinzi. Urai wao haijathibitisha.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ubelgiji, watu wawili walikua katika gari wakirejea kutoka Paris, walikaguliwa Jumamosi asubuhi katika eneo la Cambrai (kaskazini mwa Ufaransa) kisha wakapatikana katika wilaya ya Molenbeek, jijini Brussels.

Mtu wa tatu aliokaguliwa katika mji wa Cambrai, ambaye aliwasilisha nyaraka kwa niaba ya Salah Abdeslam, ameonekana kuwa aliponea chupuchupu kukamatwa na polisi wa Ufaransa Jumamosi asubuhi wakati wa ukaguzi wa barabarai katika katika mji huo wa Cambrai.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.