Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Ubelgiji: operesheni ya polisi yaendelea Brussels

Picha ya Abdeslam Salah iliyorushwa hewani na polisi ya Ufaransa kama sehemu ya kutoa wito kwa mashahidi, Novemba 15, 2015.
Picha ya Abdeslam Salah iliyorushwa hewani na polisi ya Ufaransa kama sehemu ya kutoa wito kwa mashahidi, Novemba 15, 2015. AFP/POLICE NATIONALE/AFP

Operesheni muhimu ya polisi inayoendelea katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels, nchini Ubelgijii, inalenga kumkamata Salah Abdeslam, mtuhumiwa muhimu anayesakwa katika uhusiano na uchunguzi wa mashambulizi ya Paris, Ofisi ya mashtaka ya Ubelgiji imetangaza leo Jumatatu kwa shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Matangazo ya kibiashara

"Ni sahihi," amejibu msemaji wa Ofisi ya mashitaka kwa swali aliloulizwa kuhusu kama operesheni hiyo inalenga kumpata Abdeslam Salah.

Msemaji wa Ofisi ya mashitaka hakua hata hivyo nauwezo wa kusema kama mtuhumiwa, analengwa na hati ya kimataifa ya kukamatwa na kuwasilishwa kama "mtu hatari", yupo katika nyumba iliyozingirwa na polisi katika wilaya ya Molenbeek.

Chanzo kutoka Ufaransa awali kililiambia shirik ala habari la AFP kwamba "uchunguzi" umekua ukifanyika " kuhusu kuwepo kwa Salah Abdeslam katika ghorofa" ya mji huo maarufu mjini Brussels, ambayo askari polisi wengi wamepelekwa, wakiandamana na maafisa wa Zima moto na timu za kutegua Mabomu.

Abdeslam Salah ni mtuhumiwa muhimu katika uchunguzi wa mashambulizi yaliyotokea jijini Paris Ijumaa usiku wiki iliyopita.

Raia huyu Mfaransa alizaliwa jijini Brussels, na kuelezwa kama mtu "hatari" na polisi wa Ufaransa katika taarifa ya kumsaka iliyorushwa hewani Jumapili jioni na kuelezwa na vyombo vya habari vya Ubelgiji kama "adui wa umma namba moja", anatuhumiwa kuhusika katika mashambulizi pamoja na ndugu zake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.