Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UHISPANIA-USALAMA-SOKA

Mchuano kati ya Ubelgiji na Uhispania waahirishwa kwa sababu za kiusalama

Mazoezi ya timu ya Uhispani mjini Brussels, Novemba 16, 2015.
Mazoezi ya timu ya Uhispani mjini Brussels, Novemba 16, 2015. REUTERS/Delmi Alvarez

Mechi ya kirafiki kati ya Ubelgiji na Uhispania ambayo ingelichezwa leo Jumanne jijini Brussels imeahirishwa kwa sababu za kiusalama, baada ya mashambulizi ya Paris, Shrikisho la Soka la Ubelgiji limetangaza

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho hili limesema katika taarifa yake kwamba limechukua uamzi huo kutokana na ushauri wa serikali ya Ubelgiji.

Polisi za Ubelgiji na Ufaransa zimekua zikimasakaza kwa dhati mtu anaye shukiwa kuhusika katika mashambulizi yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu 130 mjini Paris, Ijumaa iliopita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.