Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Abaaoud, muhusika mkuu katika mashambulizi ya Paris, auawa

Abdelhamid Abaaoud, asadikiwa kuuawa kwa mujibu wa gazeti la Washington Post.
Abdelhamid Abaaoud, asadikiwa kuuawa kwa mujibu wa gazeti la Washington Post. /Photo d'archives issue des réseaux sociaux/REUTERS

Abdelhamid Abaaoud, anayetuhumiwa kuwa muhusika mkuu wa mashambulizi yaliyotokea jijini Paris usiku wa Ijumaa Novemba 13, anasadikiwa kuwa ameuawa, gazeti la Washington Post limearifu Jumatano hii likinukuu vyanzo viwili vya Idara ya Ujasusi.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Washington Post alikutoa maelezo yoyote ya ziada.

Hata hivyo Kiongozi Mkuu wa mashtaka François Molins amesema kuwa polisi hawakufanikiwa kumpata mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa jijini Paris wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 129 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa.

Molins amewaambia waandishi wa habari jijini Paris kuwa mshukiwa huyo Abdelhamid Abaaoud hakuwepo katika makaazi ya Saint Denis Kaskazini mwa Paris walikofanya msako Jumatano wiki hii na haifahamiki kwa sasa yuko wapi.

Imeelezwa kuwa polisi walitumia zaidi ya risasi elfu tano kutekekeza operesheni hiyo na jumba walikokuwa wanajificha washukiwa hao ipo katika hatari ya kuporomoka.

Washukiwa nane walikamatwa, saba wakiume na mmoja wa kike lakini mwanamke mmoja alijipua wakati wa operesheni hiyo.

Rais François Hollande amesema nchi yake itafanya kile kilicho ndani ya uwezo wake kulimaliza kundi la Islamic State lilitokeleza shambulizi hilo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.