Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

François Hollande aungwa mkono na Barack Obama

François Holland na Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Novemba 24, 2015.
François Holland na Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Novemba 24, 2015. AFP/AFP

Rais wa Ufaransa François Hollande amewasili nchini Marekani Jumanne hii Novemba 24, na amekutana na mwenyeji wake rais Barrack Obama kujadiliana mbinu za kupambana na ugaidi duniani baada ya shambulizi la jijini Paris.

Matangazo ya kibiashara

"Sisi wote ni wa Ufaransa", amesema Obama kwa Kifaransa akiambatana na rais wa Ufaransa François Hollande, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Jumanne hii katika Ikulu ya White House.

Ziara hii inakuja baada ya Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kuzuru Paris Jumatatu wiki hii na kufanya mazungumzo na Rais Hollande na kuahidi kuwa nchi yake itashirikiana na Ufaransa kupambana na ugaidi.

Siku kumi na moja baada ya mashambulizi mabaya zaidi kufanyika nchini Ufaransa, Rais Obama amesema Marekani na Ufaransa "wameungana" na "wameshikamana kikamilifu" katika vita dhidi ya ugaidi.

"Tunawapenda Wafaransa", Rais Obama amesema, huku akikumbusha kwamba Ufaransa ni mshirika wa zamani wa "Marekani", akimaanisha Mapinduzi ya Marekani ya karne ya 18 ikisaidiwa na Ufaransa na Ufaransa ilikua bega kwa bega na Marekani katika mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huku ikisema "Sisi wote ni Wamarekani."

Rais wa Marekani pia amehakikisha kwamba Wamarekani hawatokubali "kunyanyasika" na vitisho vya ugaidi, siku moja baada ya tahadhari ya kimataifa iliyotolewa na Marekani kuhusu hatari ya kusafiri nje ya nchi kwa wananchi wake.

Rais Hollande pia atazuru Urusi kwenda kukutana na rais Vladimir Putin na baadaye Ujerumani kuzungumza na Kansela Angela Merkel.

Lengo ni kutafuta muungano wa kupambana na kundi la Islamic State magaidi wanaoendelea kutishia usalama wa dunia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.