Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Ukraine: EU yaongeza miezi 6 kwa vikwazo vyake vya kiuchumi dhidi ya Urusi

EU yaendelea kuibana kiuchumi Urusi kutokana na ushiriki wake katika mgogoro mashariki mwa Ukraine
EU yaendelea kuibana kiuchumi Urusi kutokana na ushiriki wake katika mgogoro mashariki mwa Ukraine AFP/AFP

Umoja wa Ulaya, kama ilivyotarajiwa, imechukua uamzi Jumatatu hii wa kuongeza miezi sita kwa vikwazo vyake vya kiuchumi dhidi ya Urusi, kwa tuma za kushiriki katika mgogoro mashariki mwa Ukraine, kwa mujibu wa taarifa rasmi.

Matangazo ya kibiashara

"Tarehe 21 Desemba 2015, Baraza la Ulaya (linalowakilisha nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya) limeongeza muda wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi hadi Julai 31, 2016", ilisema taarifa hiyo.

Vikwazo hivyo vilichukuliwa Julai 31, 2014 kwa kipindi cha mwaka mmoja "katika kukabiliana na vitendo vya Urusi mashariki mwa Ukraine",taarifa hiyo imeongeza.

Vikwazo hivyo vilikua viliongezwa muda wa miezi sita tangu tarehe 22 Juni mpaka Januari 31, 2016.

Uamuzi huu uliyokuwa ukisubirirwa, mabalozi 28 wa nchi wanachama wa EU walitoa makubaliano yao Ijumaa kwa ajili ya kuongezwa kwa muda huo.

Vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya vinalenga sekta kubwa ya uchumi wa Urusi, kama vile sektabenki, ulinzi na mafuta.

EU pia imetoa majina ya baadhi ya viongozi wa Urusi na Ukraine wanaolengwa na vikwazo vya kupigwa marufuku ya kusafiri katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na kuzuia mali zao kutokana na kuhusika katika machafuko yanayoendelea nchini Ukriane.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.