Pata taarifa kuu
UGIRIKI-PALESTINA-USHIRIKIANO

Ugiriki: Bunge lapiga kura katika neema ya utambuzi wa Palestina

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas (kushoto) na Waziri mkuu Ugiriki Alexis Tsipras, Athens, Desemba 21, 2015.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas (kushoto) na Waziri mkuu Ugiriki Alexis Tsipras, Athens, Desemba 21, 2015. ARIS MESSINIS/AFP

Jumanne hii, Bunge la Ugiriki limepitisha azimio linalotolea wito serikali ya Ugiriki kutambua taifa la Palestina wakati wa kikao maalum mbele ya Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, ambaye yuko katika ziara rasmi mjini Athens.

Matangazo ya kibiashara

Vyama vyote vyenye wajumbe katika Bunge la Ugiriki vimepiga kura katika neema ya kifungu hiki kinachotolea wito serikali ya Ugiriki "kukuza taratibu sahihi kwa kutambua taifa la Palestina na juhudi zote za kidiplomasia kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya amani" katika ukanda wa Mashariki ya Kati, Spika wa Bunge Nikos Voutsis, amesema.

Kwa upande wake, Tassos Kourakis, makamu wa Spika wa Bunge, kura hii ni "hatua muhimu katika utambuzi wa taifa la Palestina."

Abbas amesema "ana furaha kubwa kujikuta katika Bunge la Ugiriki, njia ya kuigwa kwa demokrasia", na ameshukuru wabunge wa Ugiriki kwa kura hii, ambayo "inachangia kwa kuunda taifa la Palestina."

Kura hii inakuja wiki moja baada ya azimio kama hilo lililopitishwa bila kupingwa na Kamati ya Ulinzi na Mambo ya Nje ya Bunge.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras alitangaza Jumatatu wiki hii baada ya mazungumzo yake na Abbas kurasimisha jina la Palestina kwenye nyaraka za Ugiriki kwa kubadilishwa na neno "Mamlaka ya Palestina", ambalo limekua likitumiwa hadi sasa.

Alexis tsipras ameahidi akisisitiza kuwa "Ugiriki imejikubalisha kuanzishwa kwa taifa sahihi la Palestina, huru na lenye kujitegemea kwa misingi ya mipaka iliyowekwa mwaka 1967 na yenye mji mkuu, Jerusalem Mashariki, nchi ambayo itaisha kwa amani na Israeli."

Bunge la Ugiriki liimeamua kufanya uchaguzi huu kama nchi nyingine za Ulaya, kama vile baraza la Seneti nchini Ufaransa, ambalo mwezi Desemba 2014 lilipitisha azimio kuhusu utambuzi wa taifa la Palestina.

Nakala iliyopitishwa na Bunge la Ugiriki ni msingi wa mfululizo wa maazimio ya kimataifa, uamuzi wa Bunge la Ulaya mwezi Desemba 2014 na kura katika mabunge ya nchi nyingine katika mwelekeo huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.