Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI

Mtu aliyeuawa na polisi alikua na hati ya Daech

Shambulo limetokea mbele ya kituo cha polisi katika eneo la Goutte d'Or. Eneo ambalo lilizingirwa mara moja na vikosi vya usalama, Januari 7, 2016.
Shambulo limetokea mbele ya kituo cha polisi katika eneo la Goutte d'Or. Eneo ambalo lilizingirwa mara moja na vikosi vya usalama, Januari 7, 2016. Reuters

Mtu aliyeuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi hii, Januari 7 katika kitongoji cha XVIII jijini Paris, mbele ya kituo cha polisi cha eneo la Goutte d'Or, ametambuliwa.

Matangazo ya kibiashara

Akijihami kwa kisu, mtu huyo alijaribu kuingia katika jengo hilo. Alikuwa amebeba karatasi yenye nembo ya "bendera ya kundi la IS" na ilikua na madai katika lugha ya Kiarabu "bila wasiwasi", kwa mujibu wa Ofisi ya mashitaka.

Hali bado ni ya kutatanisha kuhusu kile kilichotokea katika kituo cha polisi cha eneo la Goutte d'Or, katika kitongoji cha XVIII jijini Paris, Alhamisi hii Januari 7. Mtu aliyejihami kwa kisu ameuawa kwa kupigwa risasi na " askari polisi waliokua wakijibu shambulio", kwa mujibu wa Wizara ya mambo ndani.

Inasemekana kuwa mtu huyo alipiga kelele akisema "Allah Akbar" akijaribu kumshambulia askari polisi. Akishukiwa kuvaa fulana yenye kulipuka, mshambuliaji huyo alifanyiwa uchunguzi awali na maafisa wanaotegua mabomu. Lakini fulana aliokua akivaa imeonekana kuwa haikua na kifaa chochote cha kulipuka.

"Nimesikia mlio wa bunduki, amesema shahidi mmoja aliyehojiwa kwa simu na RFI. Nilikwenda kuchungulia dirishani; tukio hilo lilitokea sehemu ya chini. Niliona askari polisi wengi wakisubiri. Muda mchache baadae askari polisi waliondoka eneo la tukio. Kisha mkuu wa polisi alipiga mayowe akiwataka askari polisi wote kujificha.mtaa ukawa patupu. Kisha walirejea hatua kwa hatua". Shule za mitaa ya 49 na 57 katia eneo la Goutte-d'Or zilifungwa, na eneo la tukio lilizingirwa na vikosi vya usalama.

Inasemekana pia kuwa mtu huyo alikua akijulikana na polisi.

Juu ya mwili wamshambuliaji huyo, polisi iligundua simu ambayo inafanyiwa uchunguzi. Uchunguzi unaendeshwa na kitengo cha polisi ya mji wa Paris cha kupambana na ugaidi pamoja na Idara ya Ujasusi ya Ufaransa, DGSI.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, mtu huyo alikuwa anajulikana na polisi kwa kosa la wizi katika mkutano mwaka 2013, kusini mwa Ufaransa. Wakati huo, alisema kuwa anaitwa Ali Sallah, mtu asiokuwa na makazi maalumu, ambaye alizaliwa mwaka 1995 katika mji wa Casablanca, nchini Morocco. Alama za vidole vyake zilihifadhiwa, vyanzo vya polisi vimebaini.

Shambulio hili la Alhamisi hii limetokea dakika chache tu baada ya rais François Hollande, kuvitakia heri za mwaka mpya vikosi vya usalama katika makao makuu ya polisi mjini Paris, ambapo ametoa wito kwa ushirikiano bora kati ya vyombo vya usalama dhidi ya tishio la kigaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.