Pata taarifa kuu
UBELGIJI-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Uwanja wa ndege wa Brussels umerudi kufanya kazi

Ubelgiji imefungua kwa mara nyingine tena uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem Jumapili hii Aprili 3.
Ubelgiji imefungua kwa mara nyingine tena uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem Jumapili hii Aprili 3. REUTERS/Yves Herman

Shughuli zimeanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem mjini Brussels, "kitovu cha pili cha Uchumi" cha Ubelgiji, siku kumi na mbili baada ya mashambulizi yalioukumba mji huo.

Matangazo ya kibiashara

Lakini ukarabati wa sehemu wanakoorodhesha abiria "utadumu miezi kadhaa," Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Brussels Arnaud Feist, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Sehemu kubwa ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Brussel (wanakoorodhesha abiria) iliharibiwa vibaya na mashambulizi yaliotokea katika uwanja huo, na kwa sasa haifanyi kazi. Kitengo cha muda kimetengwa kwa kazi hiyo lakini kitakua na uwezo wa kuorodhesha abiria 800 kwa saa moja, sawa na 20% ya uwezo katika nyakati za kawaida.

Ndege tatu hata hivyo ziliruhusiwa kuondoka Jumapili hii ili kuonyesha kuwa uwanja huo wa ndege umerudi kufanya kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Brussels amesema kuwa uharibifu mkubwa ulifanyika katika sehemu wanako orodhesha abiria, na ndio maana imechukua siku kumi na mbili ili uwanja huo urudi kufanya kazi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.