Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Paris: Salah Abdeslam asikilizwa Ufaransa

Askari wa kikosi cha BRI kimetumwa pembezoni mwa Mahakama mjini Paris ambako Salah Abdeslam anasikilizwa na majaji Jumatano hii Aprili 27, 2016.
Askari wa kikosi cha BRI kimetumwa pembezoni mwa Mahakama mjini Paris ambako Salah Abdeslam anasikilizwa na majaji Jumatano hii Aprili 27, 2016. REUTERS/Christian Hartmann

Salah Abdeslam, mmoja wa watu walioendesha mashambulizi katika mji wa Paris alie hai amewasili nchini Ufaransa Jumatano asubuhi. Alihamishwa kutoka Ubelgiji ambako alikuwa akizuiliwa tangu kukamatwa kwake Machi 18 katika kata ya Molenbeek.

Matangazo ya kibiashara

Salah Abdeslam kwenye picha iliyorushwa na polisi wa Ubelgiji Novemba 17.
Salah Abdeslam kwenye picha iliyorushwa na polisi wa Ubelgiji Novemba 17. AFP PHOTO / HO / FEDERAL POLICE OF BELGIUM

Abdeslam Salah, mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, amefanyiwa uchunguzi Jumatano hii, kuhusu hasa kosa la mauaji yenye uhusiano ya kundi la kigaidi na kushirikiana na wahalifu, mwanasheria wake Frank Berton na mwendesha mashitaka wa mji wa Paris wametangaza.

Anashitakiwa kwa kosa la mauaji na jaribio la mauaji kwa kundi lililoandaliwa katika uhusiano na kundi la kigaidi, kushiriki katika kundi la wahalifu kwa lengo la maandalizi ya uhalifu mmoja au zaidi kwa usalam wa raia, na majaribio ya mauaji kwa kundi lililoandaliwa dhidi ya watu waliopewa mamlaka ya umma, mwendesha mashitaka wa mji wa Paris, François Molins, amesema katika taarifa yake.

Pia amefanyiwa uchunguzi kuhusu mashitaka ya "kubomoa", katika mashambulizi dhidi ya ukumbi wa tamasha wa Bataclan, kumiliki vitu vya hatari au vilipuzi, na kumiliki silaha, vyote katika kundi lililoandaliwa na kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi.

"Salah Abdeslam amewekwa rumande kwa muda katika eneo la Fleury-Mérogis. Na tayari amepelekwa eneo hilo. Jaji amemueleza kuwa atatengwa wafungwa wengine katika jela hilo," mwanasheria wake Frank Berton amebainisha.

"Kwa sasa (amesema kwamba) atataka asalie kimya, na huenda akajieleza baadaye na amechoka kutokana na safari aliyoifanya kutoka Ubelgiji," mwanasheria amesema, na kuongeza kuwa "atahojiwa Mei 20 katika undani wa kesi hiyo. "

Mashambulizi yaliotokea tarehe 13 Novemba katika mji wa Paris na Saint-Denis yaligharimu maisha ya watu 130 na wengine wengi kujeruhiwa.

                                       Magaidi wa mashambulizi ya Ufaransa

Kutoka kushoto kwenda kulia, juu hadi chini: Abdelhamid Abaaoud, Salah Abdeslam, Mohammed Merah, Chérif na Saïd Kouachi pamoja na Khaled Kelkal.
Kutoka kushoto kwenda kulia, juu hadi chini: Abdelhamid Abaaoud, Salah Abdeslam, Mohammed Merah, Chérif na Saïd Kouachi pamoja na Khaled Kelkal. DR

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.