Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA

Wakuu wa nchi za EU wanakutana kujadili Uingereza kujitoa kwenye umoja wao

Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk, waziri mkuu wa Sweden Stefan Lofven, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Slovenia Miro Cerar wakati walipokutana hivi karibuni.
Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk, waziri mkuu wa Sweden Stefan Lofven, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Slovenia Miro Cerar wakati walipokutana hivi karibuni. REUTERS/Dylan Martinez

Wakuu wa nchi kutoka jumuiya ya umoja wa Ulaya wanatarajia kuonesha mshikamano wao wakati wa mkutano wao Jumamosi hii ambapo wataidhinisha mpango wa maelekezo ya miaka miwili kwa nchi ya Uingereza kujitoa kwenye umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Wakuu hao kutoka nchi 27 zilizosalia wanatarajiwa kuitaka Uingereza kutatua masuala muhimu kuhusu kujitoa kwake kunakohusu watu, fedha na Jamhuri ya Ireland kabla ya kufanyika kwa mazungumzo yoyote ya baadae.

Mkutano huu unafanyika huku joto la kujitoa kwa Uingereza likiwa linapanda pamoja na vita ya meneno kati ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuhusu majadiliano.

Rais wa umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema kwenye barua yake kwa wakuu hao wa nchi kuwa “kabla ya kujadili mustakabali wa baadae, ni lazima kwanza tutatue tofauti zetu za zamani” akiwapa wito wa kuungana kwenye masuala ya msingi.

Viongozi hao pia wanatarajia kuunga mkono wazo wa nchi ya Ireland Kaskazini kuwa mwanachama wa umoja huo ikiwa itaungana na Ireland na kuitaka Uhispania kuwa na usemi kuhusu athari za eneo la Gibraltar.

Viongozi hawa pia kwa mara ya kwanza watajadili athari za Uingereza kujitoa, makao mapya ya benki za Ulaya ambazo kwa sasa zina makao jijini London.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.