Pata taarifa kuu
WHO-UINGEREZA-CANADA

WHO yakosolewa kumteua Mugabe kuwa balozi wa afya

Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe
Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe Jekesai NJIKIZANA / AFP

Mkuu wa shirika la afya la kimataifa anataraji kubadili upya uteuzi wa raisi Mugabe wa Zimbabwe kuwa balozi mwema wa shirika hilo kufuatia ukosolewaji uliotolewa kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Tedros Adhanom mkuu wa WHO alimteua raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe kuwa balozi wa afya baada ya kuisifu Zimbabwe kuzingatia afya ya umma.

Serikali ya Uingereza na Canada zimeshtushwa na uamuzi huo uliofanywa na shirika la afya la kimataifa na kusema haukubaliki,huku wakosoaji wakibainisha kasoro katika mfumo wa huduma za afya nchini Zimbabwe chini ya utawala wa raisi Mugabe.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema taarifa za uteuzi huo alizipokea kwa kustaajabu akifikiri ni sikukuu ya wajinga ambayo hufanywa kila April.

Amedai kuwa utawala wa Mugabe unashutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu hivyo uteuzi huo sio sahihi kwake na haukubaliki kwa kuwa uko kinyume la lengo la kimataifa la kulinda utu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.