Pata taarifa kuu
ITALIA-UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Italia wanapiga kura kuwachagua wabunge wapya

Makaratasi ya kupigia kura wakati wa Uchaguzi wa wabunge Machi 04 2018
Makaratasi ya kupigia kura wakati wa Uchaguzi wa wabunge Machi 04 2018 Andreas SOLARO / AFP

Raia wa Italia wanapiga kura kuwachagua wabunge wapya, katika Uchaguzi ambao muungano wa vyama vya mrengo wa kulia huenda ukashinda.

Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi saa za jiji kuu Roma,  na vitafungwa saa tano usiku, huku matokeo rasmi yakitarajiwa kufahamika siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, matokeo ya awali yanatarajiwa kufahamika punde tu vituo vya kupigia kura vitakapofungwa.

Mshindi anatarajiwa kupata asilimia 40 ya viti bungeni kati ya 315 vinavyowaniwa ili kuunda serikali.

Iwapo muungano huo utashinda, mwanasisasa mkongwe ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu Silvio Berlusconi mwenye umri wa miaka 81, hawezi kuongoza serikali  kwa sababu ya amezuiwa kushika madaraka katika Ofisi ya umma hadi pale adhabu ya kukwepa kulipa kodi itakapomalizika mwaka ujao.

Ushindani hata hivyo pia unatoka kwa Waziri Mkuu wa zamani Matteo Renzi kutoka chama cha Democratic.

Raia wa Italia wanapiga kura huku wakisumbuliwa na changamoto za kiuchumi, ajira na wimbi la wakimbizi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.