Pata taarifa kuu
EU-UTURUKI

EU na Uturuki zashindwa kukubaliana namna watakavyoshirikiana

Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk, rais wa Uturuki Recep Erdogan na mkuu wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker wakiwa mjini Varna, Bulgaria. 26 Machi 2018.
Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk, rais wa Uturuki Recep Erdogan na mkuu wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker wakiwa mjini Varna, Bulgaria. 26 Machi 2018. REUTERS/Stoyan Nenov

Umoja wa Ulaya umesema umeshindwa kufikia suluhu yoyote na nchi ya Uturuki katika mazungumzo yao na rais Recep Tayyip Erdogan mazungumzo yaliyolenga kujaribu kujenga upya uhusiano wao.

Matangazo ya kibiashara

Rais Erdogan alifanya mazungumzo katika chakula cha usiku na rais wa tume ya Ulaya Donald Tusk pamoja na mkuu wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker mjini Bulgaria huku masuala ya uhusiano wa nchi yake na umoja huo ikiwa ni ajenda kubwa.

Mjadala ulikuwa ni operesheni inayoendelea kufanywa na rais Erdogan dhidi ya wale anaowaita wasaliti na walioandaa mapinduzi yaliyoshindikana mwaka 2016, kukamatwa kwa waandishi wa habari, operesheni za jeshi la Uturuki dhidi ya Wakurdi kaskazini mwa Syria na hatua ya nchi hiyo kusitisha ubadilishanaji wa wahamiaji ni masuala yaliyojadiliwa.

Hatua hizi zimesababisha kuongezeka kwa joto la uhusiano baina ya nchi za Ulaya na Uturuki na hata kufanya mchakato wa nchi hiyo kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya kuelekea kugonga ukuta kabisa.

Jumatatu ya wiki hii rais Erdogan alisisitiza utayari wa nchi yake kujiunga kwenye umoja wa Ulaya, ombi ambalo kwa muda sasa viongozi wa Ulaya wamekuwa hata hawalijadili kwenye mikutano yao.

Hata hivyo licha ya mazungumzo yaliyotarajiwa kutoka na maazimio yenye tija, rais Tusk anasema hawakufanikiwa kukubaliana chochote.

Tusk amesema masuala ambayo mpaka sasa hayajapata muafaka ni pamoja na suala la demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na mashambulizi ya Uturuki kwenye ardhi ya Syria.

Licha ya viongozi wa Ulaya kuonesha kutokuwepo kwa mwangaza wowote wa kufikia makubaliano, rais Erdogan mwenyewe amewaambia waandishi wa habari kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufikiwa muafaka na nchi yake kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.