Pata taarifa kuu
UFARANSA-UHAMIAJI-USALAMA

Mgawanyiko wajitokeza kufuatia kupitishwa kwa sheria ya uhamiaji Ufaransa

Baada ya mjadala uliodumu zaidi ya masaa 60, Bunge la Ufaransa lilipitisha sheria tata ya uhamiaji, Jumapili, Aprili 22.
Baada ya mjadala uliodumu zaidi ya masaa 60, Bunge la Ufaransa lilipitisha sheria tata ya uhamiaji, Jumapili, Aprili 22. REUTERS/Stephane Mahe

Bunge nchini Ufaransa limepitisha sheria tata ya uhamiaji ambayo imedhihirisha mgawanyiko usio wa kawaida katika chama cha rais Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya takribani saa 61 za mjadala sheria hiyo iliidhinishwa kwa kura 228 huku 139 zikishindwa kuipinga na kura 24 kutopigwa.

Kwa kiasi kikubwa ilipitishwa na wafuasi wanaomuunga mkono raisi Macron lakini kaimu kiongozi wa chama cha macron Jean-Michel Clement, aliasi na kutangaza kukacha chama cha raisi huyo baada ya kupig akura ya hapana kwa muswada huo.

Upinzani ulidhihirika kutoka kwa wabunge wa Vyama vyote vya mrengo wa kulia na kushoto lakini pia chama chake Marine le pe, National Front.

Bunge la kawaida la Ufaransa lilipaswa kupigia kura muswada huo mnamo ijumaa lakini mjadala mkali ulilazimisha zoezi hilo kuingia weekend kutokana na marekebisho zaidi ya elfu moja kupendekezwa na manaibu.

Zaidi ya mabadiliko mia mbili yalipendekezwa na upande wa chama cgha macron wakati wabunge wa macron waziwazi waliukosoa mpango wake wa kuongeza muda zaidi kwa wahamiaji kukaa katika kambi kwa siku 90.

serikali imeutetea muswada huo ingawa imekosolewa na mrengo wa kulia.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.