Pata taarifa kuu
UFARANSA-URUSI-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais wa Ufaransa aalikwa katika mkutano kuhusu Uchumi St. Petersburg

Marais wa Ufaransa na Urusi Vladmiri Putin na Emmanuel Macron Mei 24, 2018 karibu na St. Petersburg.
Marais wa Ufaransa na Urusi Vladmiri Putin na Emmanuel Macron Mei 24, 2018 karibu na St. Petersburg. Dmitry LOVETSKY / POOL / AFP

Kwa siku ya pili ya ziara yake ya nchini Urusi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakuwa mgeni heshima Ijumaa wiki hii katika mkutano kuhusu Uchumi katika mji wa St Petersburg, ambapo ataambatana na ujumbe mkubwa wa viongozi wa makampuni makubwa ya Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo hukusu Uchumi utakaofanyika katika mji wa St. Petersburg, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anabeba ujumbe ulio wazi: Ufaransa inataka kuendelea kufanya biashara nchini Urusi licha ya mvutano wa kidiplomasia katika miaka ya hivi karibuni.

Rais Macron pia amekumbusha kwamba Ufaransa imebaki kuwa mojawapo ya washirika wakuu wa biashara ya Urusi licha ya vikwazo vilivyopitishwa baada ya kuunganisha Crimea kwa Urusi. Kwa jumla, mikataba hamsiniinatarajiwa kusainiwa leo Ijumaa Mei 25.

Kwa upande wa Urusi, wanakaribisha uwepo wa Emmanuel Macron katika mkutano huu. Hii ni ishara kwamba Urusi inachukuliwa kama mshirika wa kawaida kwa hali yoyote ya kiuchumi, vyombo vya habari vya Urusi vimearifu.

Vladimir Putin anaweza tu kufurahia katika hali yoyote ziara hii ya kiongozi wa Ulaya katika mkutano huu. Uchumi wa Urusi unaimarika baada ya miaka kadhaa nchi hiyo ikikabiliwa na mdororo mkubwa wa uchumi.

Kremlin kwa sasa ina wasiwasi juu ya matokeo ya vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani ambavyo vinaweza kutishia ushirikiano huu na Ufaransa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.