Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SIASA

Pedro Sanchez amrithi Mariano Rajoy aliyetimuliwa na Bunge

Pedro Sanchez waziri mkuu mpya wa Uhispania.
Pedro Sanchez waziri mkuu mpya wa Uhispania. Emilio Naranjo/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, ametimuliwa Ijumaa wiki hii kwenye wadhifa wake kufuatia kashfa ya rushwa. Wakati huo huo bunge la nchi hiyo limemepitisha Pedro Sanchez kuchukua nafasi ya waziri mkuu.

Matangazo ya kibiashara

edro Sanchez amemrithi mtangulizi wake Mariano Rajoy,baada ya kutimuliwa katika kura ya kutokua na imani naye iliyopigwa na bunge Ijumaa hii Juni 1. Mariano Rajoy aliondolewa kwa kura 180 dhidi ya kura 169, huku mbunge mmoja akijizuia kupiga kura.

Hatua hii imekuja baada ya chama cha Mariano Rajoy kushtumiwa kashfa ya rushwa iliyoitwa "Gürtel".

Muda mfupi kabla ya kupiga kura, Mariano Rajoy, alikubali kushindwa. "Tunaweza kufikiria kwamba kura ya kutokua na imani itapitishwa na bunge. Matokeo yake, Pedro Sanchez atakuwa kiongozi mpya wa serikali, "alisema, kwa hotuba fupi mbele ya wafuasi wake. Alimpongeza mpinzani wake na kusisitiza kuhusu "heshima" yake kwa kuongoza nchi hiyo.

Mariano Rajoy alikua madarakani tangu mwezi Desemba 2011, na uongozi wake ulikumbwa na migogoro kadhaa mikubwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.