Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-WAHAMIAJI

Merkel na Macron kuzungumzia suala la mgogoro wa wahamiaji

Emmanuel Macron na Angela Merkel wakati wa mkutano uliopita huko Berlin, mnamo mwezi Aprili.
Emmanuel Macron na Angela Merkel wakati wa mkutano uliopita huko Berlin, mnamo mwezi Aprili. Kay Nietfeld/Pool via Reuters

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kufanya ziara leo Jumanne nchini Ujerumani katika mkutano kati ya Ufaransa na nchi hiyo. Mkutano kati ya viongozi wa nchi hizi mbili utajikia hasa kuhusu mgogoro wa wahamiaji barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Siku kumi kabla ya kikao cha Baraza la Ulaya, mkutano kati ya Angela Merkel na Emmanuel Macron ulitazamiwa awali kujikita katika suala la mpango wa nchi hizi mbili kuhusu marekebisho ya eneo la nchi zinazotumia euro. Lakini suala la meli ya Aquarius iliyokua ikibeba wahamiaji 630 ambayo ilikataliwa kutia nanga nchini Italia na Malta limepewa kipaumbele katika mkutano kati ya viongozi hawa wawili. Katika mkutano wa leo Jumanne, watazungumzia kuhusu mgogoro wa wahamiaji unaoikumba Ulaya wakati huu.

Mgogoro wa wahamiaji ni muhimu, hasa kwa Angela Merkel ambaye amedhoofika kisiasa kutokana na suala hili.

Angela Merkel ana hamu ya kupata suluhisho la Ulaya kwa changamoto ya suala la uhamiaji ikiwa anataka kuepuka mgogoro mkubwa katika nchi yake. Kama Emmanuel Macron, anaamini kuwa sera ya uhamiaji inaweza kuamuliwa tu na kutekelezwa kwa ufanisi katika ngazi ya Ulaya.

Lakini Umoja wa Ulaya umegawanyika juu ya suala hilo. Mageuzi ya mfumo wa Ulaya wa kutoa hifadhi kwa wakimbizi umesimama kwa miaka miwili. Ili kuikoa Italia na Ugiriki kwa wimbi la wakimbizi, nchi, Tume ya Ulaya inapendekeza kugawana moja kwa moja wakimbizi wanaowasili katika baadhi ya nchi za Ulaya wakati wa migogoro.

Wakati huo huo, Ufaransa na Ujerumani wanatarajia kutoa wito wa kuimarisha ulinzi mkali kwenye mipaka na kuipa uwezo wa kutosha idara inayohusika na ulinzi katikka mipaka ya nchi za Ulaya (Frontex). Mazungumzo yatachukua muda mrefu. Mkutano huu kati ya Angela Merkel na Emmanuel Macron, yanatarajiwa kuanza leo mchana, na yatadumu saa nne.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.