Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA-UCHUMI

Viongozi wa waandamanaji wajiondoa kwenye mazungumzo na serikali Ufaransa

Waandamanaji waaanza kufikishwa mahakamani kufuatia machafuko Desemba 1 mjini Paris.
Waandamanaji waaanza kufikishwa mahakamani kufuatia machafuko Desemba 1 mjini Paris. Abdulmonam EASSA / AFP

Viongozi wa waandamanaji nchini Ufaransa, ambao wamakuwa wakindaa maandamano nchini humo kulalamikia kuongezwa kwa kodi ya mafuta, wamesema hawatashiriki katika mazungumzo na Waziri Mkuu Edouard Philippe.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika leo Jumanne, huku viongozi wa waandamanaji hao wakisema wamepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa waandamanaji ambao wamewataka kutoshiriki katika mazungumzo hayo na serikali.

Maandamano haya yamekuwa yakifanyika tangu katikati ya mwezi Novemba na sasa yamegeuka kuwa makabiliano makali kati ya waandamanaji na Polisi.

Rais Emmanuel Macron amekuwa akisema, anawaelewa waandamanaji hao lakini hawezi kuondoa nyongeza hiyo iliyosababisha bei ya mafuta kupanda.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.