Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-THERESA MAY

Waziri Mkuu May aomba miezi mitatu zaidi Uingereza ijiondoe EU

Waziri Mkuu wa  Theresa May akizungumza na wanahabari tarehe 20 mwezi Machi 2019
Waziri Mkuu wa Theresa May akizungumza na wanahabari tarehe 20 mwezi Machi 2019 Jonathan Brady/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amewaomba viongozi wa Umoja wa Ulaya kukubali nchi yake ijiondoe kwenye  huo baada ya miezi mitatu.

Matangazo ya kibiashara

Iwapo ombi hilo litajadiliwa na kuamuliwa na viongozi wa Umoja huo watakapokutana mwishoni mwa wiki hii, basi nchi hiyo itajiondoa ifikapo mwisho wa mwezi Juni.

Hii imekuja, baada ya wabuge kukataa mapendekezo ya serikali kuhusu namna mambo yatakavyokuwa iwapo itajiondoa kwenye mkataba huo, uliokubaliwa kati ya viongozi wa EU na Uingereza.

Wiki iliyopita, wabunge walikataa mapendekezo mapya lakini pia wakapinga  kujiondoa kwenye Umoja huo bila ya mkataba.

Uingereza ilitarajiwa kujiondoa kwenye Umoja huo ifikapo Juni 29 lakini, haitawezekana baada ya mkataba kukataliwa na wabunge.

Waziri Mkuu May, amewashtumu wabunge kwa kuchelewesha  matamanio ya raia wa Uingereza waliamua mwaka 2016 kuwa wanataka kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.