Pata taarifa kuu
UMOJA WA ULAYA-SIASA-UINGEREZA

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubali ombi la Uingereza kuhusu kujiondoa EU

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May Reuters TV via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anarejea nchini Uingereza kuwashawishi wabunge kuunga mkono mkataba wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, baada ya viongozi wa Umoja huo kukubali kuiongezea muda wa kujiondoa.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo ya saa nane kati ya Waziri Mkuu May na viongozi wa EU, ilikubalika kuwa muda wa kujiondoa uongozwe hadi tarehe 22 mwezi Mei na sio tarehe 29 mwezi Machi kama ambavyo ilivyokuwa imekubaliwa.

Wiki ijayo, Waziri Mkuu May atawasilisha mkataba bungeni ili wabunge waupigie tena kura, lakini hadi sasa haijawa wazi kuhusu msimamo wa wabunge kuhusu muda waliopewa.

Hata hivyo, May amesema kuwa kwa sasa wabunge wana uchaguzi  wazi mbele yao kuukubali mkataba huo au kuukata.

“Nitafanya bidii ili kuhakikisha kuwa nawashawishi wenzangu kupata uungwaji mkono,” alisema.

Wabunge watakuwa na nafasi nyingine, kupiga kura kwa mara ya tatu wiki ijayo licha ya spika John Bercow kusema kutoa wito wa serikali kuja na mapendekezo ambayo wabunge hawatayakataa.

Iwapo mkataba hautapitishwa, Uingereza huenda ikajiondoa kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo tarehe 12 mwezi Aprili bila ya mkataba.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.