Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Brexit: Wabunge wa Uingereza wafutilia mbali mapendekezo kadhaa ya kujiondoa EU

Spika wa baraza la wawakilishi John Bercow akitangaza matokeo ya kura za wabunge kuhusu mapendekezo nane ili kupata suluhisho mbadala wa kujitoa Umoja wa Ulaya.
Spika wa baraza la wawakilishi John Bercow akitangaza matokeo ya kura za wabunge kuhusu mapendekezo nane ili kupata suluhisho mbadala wa kujitoa Umoja wa Ulaya. Reuters TV via REUTERS

Wabunge wa Uingereza wamepiga kura Jumatano wiki hii dhidi ya mapendekezo nane ya kupata suluhisho mbadala ya mkataba wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu uliofikiwa kati ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na Brussels kwa niaba ya Umoja wa Ulaya ulikataliwa mara kadhaa na bunge la Uingereza.

Kujiondoa bila mkataba, umoja wa forodha kwa mapoja na Umoja wa Ulaya, kukataa kujitoa katika Umoja wa Ulaya ikiwa hakutakuwa na mkataba wowote ambao ulipitishwa na wabunge, ni miongoni mwa matukio haya, ambayo wao wenyewe yalipendekeza.

Kukataliwa kwa kupitisha mapendekezo haya haishangazi wakati bunge lenyewe limegawanyika.

Hata hivyo kuna baadhi ya wabunge ambao wamemtaka Waziri Mkuu Theresa May ataje siku atakayojiuzulu.

Kwa upande wa Waziri wa masuala ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya amesema: "Hakuna uwezekano mwengine ulio wazi kwa mkataba uliopendekezwa na Waziri Mkuu, kwa hiyo ni mkataba huo ulio fikiwa na kutiwa saini na Umoja wa Ulaya ambao Bunge linapaswa kuunga mkono".

Iwapo mkataba huo hautapitishwa, kuna hatari ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo bila ya mkataba wowote.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.