Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Wabunge wapiga kura dhidi ya mapendekezo mbadala ya makubaliano ya Brexit

John Bercow, Spika wa baraza la wawakilishi akitangaza matokeo ya uchaguzi wa mapendekezo manne mbadala kwa makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya yaliyofikiwa kati ya serikali yaUingereza na Brussels, London, 1 Aprili 2019.
John Bercow, Spika wa baraza la wawakilishi akitangaza matokeo ya uchaguzi wa mapendekezo manne mbadala kwa makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya yaliyofikiwa kati ya serikali yaUingereza na Brussels, London, 1 Aprili 2019. Reuters TV via REUTERS

Bunge la Uingereza limepiga kura dhidi ya mapendekezo manne mbadala kwa makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, yaliyofikiwa kati ya serikali ya nchi hiyo na Brussels, mkataba ambao tayari wamefutilia mbali mara tatu.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kupiga kura dhidi ya mapendekezo 8 mbadala wiki iliyopita, wabunge wamefutilia mbali mapendekezo mapya ambayo yamekuwa yamependekeza kuendelea na uhusiano wa karibu na Umoja wa Ulaya au kusitisha mchakato wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila mkataba Aprili 12.

Waziri wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Stephen Baclay, amesikika akisemakuwa kufuatia hali hiyo inayoendelea kujitokeza, kunahatari Uingereza ijitoe katika Umoja wa Ulaya bila mkataba ndani ya siku kumi na moja zijazo.

Wadadisi wanasema kujitoa kwa Uingereza kumechangiwa kwa sehemu kubwa na kile ninachoendelea Ulaya ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa na tabia ya kupenda siasa za kihafidhina, za uzalendo , kuzuia mwingiliano na wengi hasa wanaotoka nje ya Ulaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.