Pata taarifa kuu
UFARANSA-DINI-MAJANGA ASILI

Notre-Dame de Paris: Viongozi wa kanisa katoliki Afrika waelezea masikitiko yao

Askofu Mkuu wa Kinshasa, Fridolin Ambongo Besungu, hapa ilikuwa Desemba 24, 2018 wakati wa misa ya Krisimasi
Askofu Mkuu wa Kinshasa, Fridolin Ambongo Besungu, hapa ilikuwa Desemba 24, 2018 wakati wa misa ya Krisimasi REUTERS/Baz Ratner

Viongozi wa kanisa katoliki kutoka katika maeneo mbalimbali duniani wamebaini maskitiko yao kutokana na kuteketea kwa moto kwa kanisa la Notre-Dame jijini Paris ambalo ujenzi wake ulianza karne ya 1163 na kudumu kwa muda wa karne mbili kabla ya kutamatika.

Matangazo ya kibiashara

Kanisa la Notre-Dame de Paris, ni moja ya makanisa maarufu, linalotembelewa zaidi nchini Ufaransa ambalo limekumbwa na mkasa wa moto ambao uliteketeza paa na sehemu ya muundo wake.

Askofu wa kanisa katoliki jijini Kinshasa Fridolin Ambongo amesema amesikitishwa na tukio hilo ambalo linatokea majuma mawili baada ya kushiriki misa katika kanisa hilo.

Maskitiko kama hayo yametolewa pia na Kadinali Sarr, askofu wa kanisa Katoliki wa jijini Dakar, ambae amesema mahujaji kutoka Dakar wamekuwa wakizuru eneo hilo kila mwaka.

Naye Askofu wa jiji la Bangui nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Dieudonné Nzapalainga amesema Notre-Dame de Paris imekuwa kama vile mama anaekutanisha wanae.

Vikosi vya zima moto vinaendelea kuzima moto huo katika kanisa hilo lililodumu kwa takriban miaka 850.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini maafisa wanauhusisha mkasa huo na shughuli ya ukarabati inayoendelea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.