Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Uingereza: Kura mpya ya wabunge kuhusu uchaguzi wa mapema kupigwa

Wabunge wa Uingereza wnatarajia kupiga kura iwapo wanataka au la uchaguzi wa mapema, uliopendekezwa na Boris Johnson.
Wabunge wa Uingereza wnatarajia kupiga kura iwapo wanataka au la uchaguzi wa mapema, uliopendekezwa na Boris Johnson. PRU / AFP

Wabunge wa Uingereza wanatarajia kupiga kura leo Jumatatu kuamua iwapo wanataka au la uchaguzi wa mapema, unaopendekezwa na Waziri Mkuu Boris Johnson ili kuodokana na mzozo wa kisiasa na kutekeleza mkakati wake wa Brexit unaoendelea kukosolewa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Boris Johnson hana tena viti vingi bungeni baada ya mbunge mmoja kujitenga naye na wabunge wengine 21wenye msimamo wa wastani kutoka chama cha Conservative kufukuzwa katika chama hicho baada ya kupiga kura na upinzani muswada kuhusu kuepuka Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.

Jambo jingine ni kwamba kaka yake mwenyewe, Jo Johnson, Alhamisi alijiuzulu serikalini akibaini kwamba hatua hiyo aliichukuwa kwa "maslahi ya kitaifa", akifuatiwa Jumamosi na Waziri wa Kazi Amber Rudd, baada ya wiki mbaya kwa Boris Johnson.

Kulingana na uchunguzi wa YouGov uliyochapishwa katika gazeti la Sunday Times, Chama cha Conservative kitaongoza kwa 35% ya kura, huku kikishinda chama cha Labour alama zaidi ya 14. Uchunguzi mwengine uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kukaribiana kwa kura kati ya vyama hivyo viwili, lakini chama cha Conservative kikiongoza.

Kwa kuandaa uchaguzi huu, Boris Johnson anahitaji theluthi mbili katika Bunge. Lakini upinzani hautaki kufanyika kwa uchaguzi huo kwa sasa.

- Ripoti "isiyo na maana" -

Boris Johnson aliingia madarakani mwezi Julai, na kuahidi kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31, kwa makubaliano au bila ya makubaliano. Amepinga tarehe mpya ya Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya, iliyopangwa hapo awali Machi 29.

Bunge lilipiga kura ya muswada wa sheria unaomlazimisha kuahirisha kwa miezi mitatu tarehe ya Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya (Brexit) ikiwa hatapata mkataba wa Uingereza kujitoa katika umoja huo ifikapo Oktoba 19, mara tu baada ya kikao cha Baraza la Ulaya cha Oktoba 17 na 18.

Lakini Boris Johnson alirejelea kauli yake katika gazeti la Sunday Express siku ya Jumapili kwamba "hatokubali kuahirishwa" kwa mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ambapo 52% ya wananchi wa Uingereza waliamua katika kura ya maoni ya Juni 2016.

Waziri Mkuu wa Uingereza "hana kabisa" nia ya kuomba kuongezwa muda wa ziada katika kikao cha Baraza la Ulaya cha tarehe 17 na 18 Oktoba, Waziri wake wa Fedha Sajid Javid, aliambia BBC.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.