Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SIASA-USALAMA

Uhispania kurudi kwenye uchaguzi kwa mara ya nne ndani ya kipindi cha miaka minne

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez mbele ya Bunge, Madrid Septemba 11, 2019.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez mbele ya Bunge, Madrid Septemba 11, 2019. REUTERS/Sergio Perez

Uhispania inajianda kurudi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu ikiwa ni mara ya nne ndani ya kipindi cha miaka minne.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja baada ya kiongozi wa serikali kutoka chama cha Kisoshalisti, Pedro Sanchez. kushindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha kwa kuendelea kushikilia nafasi yake.

"Nchi imekaribia (kuandaa) uchaguzi mpya mnamo Novemba 10," Sanchez amekiri Jumanne wiki hii baada ya kupokelewa na Mfalme wa Uhispania Felipe wa 6, ambaye alikuwa akifanya mazungumzo tangu Jumatatu, ili kutafutia ufumbuzi swala hilo.

"Matokeo (ya mazungumzo ya mfalme) yako wazi: hakuna wingi wa viti katika bunge la taifa ambao unaweza kupelekea kuundwa kwa serikali," ameongezea Bw Sanchez, ambaye alishinda uchaguzi uliopita wa Aprili 28 lakini bila kupata wingi wa viti bungeni.

"Nilijaribu kwa njia zote lakini kazi yangu iliambulia patupu," Bw Sanchez ameongeza, akimaanisha wapinzani wake ambao walimshtumu tangu mwanzo kwamba anataka uchaguzi mpya.

Mapema ofisi ya Mfalme ilibaini kwamba Mfalme hatapendekeza mgombea kwenye nafasi ya kiongozi wa serikali, hakuna "anaetimiza idadi ya viti vinavyohitajika katika Bunge la taifa."

Uhispania inaendelea kukumbwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa tangu kuvujinka kwa muungano wa vyama viwili vyenye wafuasi wengi mnamo mwaka wa 2015 na kuingia katika Bunge chama cha mrengo wa kushoto chenye itikadi kali cha Podemos na kile cha Ciudadanos. Kwa sasa Bunge la Uhispania Bunge limegawanyika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.