Pata taarifa kuu
Ufaransa-CHIRAC-SAIASA-USALAMA

Rais wa zamani wa Ufaransa azikwa

Jeneza la Jacques Chirac, katika kanisa la Paris la Saint-Sulpice, Septemba 30, 2019.
Jeneza la Jacques Chirac, katika kanisa la Paris la Saint-Sulpice, Septemba 30, 2019. Francois Mori / POOL / AFP

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac, amezikwa katika makaburi ya watu mashuhuri ya Montparnasse Kusini kwa jiji la Paris, kabla ya zoelzi hilo, kulikuwa na ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dunia.

Matangazo ya kibiashara

Imekuwa ni siku yenye huzuni kwa wananchi wa Ufaransa, waliojitokeza katika barabara za jiji la Paris, kumuaga kiongozi wao wa zamani, aliyekuwa rais wao, Waziri Mkuu na Meya wa jiji la Paris.

Chirac ni rais aliyependwa na wengi ndani na nje ya Ufaransa, na leo nchini Ufaransa, imekuwa ni siku ya kitaufa ya kumkumbuka kiongozi huyo wa zamani aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 86.

Katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Sulpice jijini Paris, viongozi wa Kanisa hilo, waliongoza misa ya kumwaga kiongozi huyo, huku viongozi waliohudhiria kama rais wa Urusi Vladimir Putin, rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na marais kadhaa kutoka mataifa ya Afrika wakionekana wenye huzuni kwa kumpoteza rafiki.

Hakuna kiongozi wa dunia, aliyetoa hotuba katika ibada hiyo, nje ya Kanisa wakati wa kwenda kumzika kiongozi huyo wa zamani, rais wa sasa Emmanuel Macron aligusa jeneza lililofunikwa bendera ya nchi hiyo lililobeba mwili wa mtangulizi wake ambaye amezikwa na heshima zote za kijeshi.

Raia wa Ufaransa na viongozi mbalimbali wa dunia, wamesema watamkumbuka Jacques Chirac kama kiongozi aliyepigania nchi yake, huku viongozi wa Afrika wakisema alipenda bara hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.