Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Maafisa wanne wa polisi wauawa katika shambulio la kisu Paris

Shambulio limetokea katika makao makuu ya polisi ya Paris, maafisa 4 wa polisi wameuawa na mshambuliaji ameuawa kwa kupigwa risasi, Oktoba 3, 2019.
Shambulio limetokea katika makao makuu ya polisi ya Paris, maafisa 4 wa polisi wameuawa na mshambuliaji ameuawa kwa kupigwa risasi, Oktoba 3, 2019. Martin BUREAU / AFP

Shambulio hilo limetokea Alhamisi hii, Oktoba 3 katika makao makuu ya polisi ya Paris, nchini Ufaransa. Polisi wanne wameuawa. Mshambuliaji, ambaye alikuwa miongoni mwa wafanyakazi kwenye makao makuu ya polisi ameuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea karibu saa saba mchana ndani ya makao makuu ya polisi jijini Paris, katika eneo la kihistori katikati mwa mji mkuu Paris. Polisi wanne wameuawa. Mtu mwingine amejeruhiwa na yuko katika hali mbaya. Amesafirishwa katika hospitali ya Mafunzo ya Jeshi, Percy.

Hijafahamika wazi jinsi shambulio hilo lilivyotokea. Shambulio liliripotiwa hapo awali katika ofisi ya mshambuliaji, ambaye ni mfanyakazi kwenye makao makuu ya polisi kwa miaka 20. Silaha inayotumiwa katika shambulio hilo ni kisu cha kauri.

Kulingana na ushuhuda wa kwanza uliokusanywa na wanahabari wa RFI, mshambuliaji alikuwa mfanyikazi mzuri.

Helikopta ya maafisa wa uokoaji iko kwenye eneo la tukio, Oktoba 3, 2019
Helikopta ya maafisa wa uokoaji iko kwenye eneo la tukio, Oktoba 3, 2019 Martin BUREAU / AFP

Waziri wa Mambo ya Ndani Christophe Castaner, Waziri Mkuu Edouard Philippe na Rais Emmanuel Macron wamezuru eneo la tukio. Polisi imezingira eneo hilo.

Wachunguzi wanachunguza uwezekano wa kuwepo mgogoro wa kibinafsi, kulingana na vyanzo vya AFP.

Kituo cha kisaikolojia kimefunguliwa katika makao makuu ya polisi ya Paris, kulingana na mwandishi wa RFI, Anne Soetemondt.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.