Pata taarifa kuu
UINGEREZA-HAKI-USALAMA

Miili 39 yapatikana katika lori Essex, Uingereza

Eneo ambapo miili 39 ilipatikana katika lori katika huko Grey jijini Essex limezingirwa na polisi ya Uingereza.
Eneo ambapo miili 39 ilipatikana katika lori katika huko Grey jijini Essex limezingirwa na polisi ya Uingereza. REUTERS/Hannah McKay

Miili thelathini na tisa imepatikana katika lori usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii katika eneo la Grey, jijini Essex, mashariki mwa London.

Matangazo ya kibiashara

Dereva, mwenye umri wa miaka 25, mwenye asili ya Ireland Kaskazini, amekamatwa kwa mauaji, polisi ya Uingereza imetangaza. Kulingana na ripoti ya awali ya uchunguzi, lori hilo lilitoka Bulgaria na liliingia Uingereza Jumamosi, Oktoba 19 likipitia Holyhead, bandari inayopatikana kwenye pwani ya magharibi mwa Uingereza.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu nchi wanakotoka waathiriwa. haijulikani ikiwa wathiriwa walikuwa wahamiaji.

"Mchakato wa kutambua miili unaendelea," mkuu wa polisi wa mji wa Essex, Andrew Mariner, amesema katika taarifa.

Wahamiaji wengi wamekuwa wakijaribu kuingia Uingereza katika miaka ya hivi karibuni kwa kujificha katika kasha za gari za mizigo au katika boti. Polisi imezingira eneo Waterglade ambapo gari hilo limeegeshwa na watu wamepigwa marufu kukaribia eneo hilo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema, "ameshtushwa" na habari hii. Ameendelea kusema, "Ninaungana kwa huzuni na familia zilizopoteza wapendwa wao. "

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.