Pata taarifa kuu
UFARANSA-MGOMO-AFYA

Mgomo waendelea katika hospitali za umma Ufaransa

Wafanyakazi wa afya wa hospitali ya Saint-Louis huko Paris wakiandamana Februari 3, 2020.
Wafanyakazi wa afya wa hospitali ya Saint-Louis huko Paris wakiandamana Februari 3, 2020. Thomas SAMSON / AFP

Hali katika hospitali za umma nchini Ufaransa inaendelea kudorora, wakati ilitakiwa kuhifadhiwa. Huu ni ujumbe ambao wale wanaotarajiwa kuandamana leo Ijumaa, Februari 14 katika maeneo mbalimbali nchini Ufaransa wanataka kufikisha.

Matangazo ya kibiashara

Mgomo ulioanza Machi 2019 katika idara ya huduma za dharura umeanza kuenea karibu katika idara zote. Licha ya jitihada za serikali, hali inaendelea kuwa mbaya katika hospitali za umma.

"Serikali inaua" hayo ni maneneo yaliyoandikwa kwenye bango jekundu lililobandikwa kwenye lango la Pitié-Salpêtrière, moja ya hospitali kubwa za mjini Paris. Katika hospitali hii sawa na hospitali zingine wagomaji wanalaani kile wanachosema ushawishi mkubwa katika nyanja ya kifedha ambao unapewa kipaumbele kuliko afya ya mgonjwa.

Kwa kukemea hali hiyo, madaktari zaidi ya 1,000 ambao ni wakuu wa idara mbalimbali katika hospitali za umaa wameamua kujiuzulu kwenye nafazi zao za kiutawala.

"Ninapofika kazini, ninajiuliza je! kutakuwa na mfanyakazi mmoja tu wa muda kwa mchana pekee katika chumba hiki cha wagonjwa walio katika hali mbaya. Kuna wauguzi ambao wanasema "kazi yangu imepoteza maadili, sina tena wakati wa kuongea na wagonjwa, nikp niko tu", amesema Agnès Hartemann ambaye ni mkuu wa idara ya ugonjwa wa kisukari katika hospitali ya Pitié-Salpêtrière na ni mmoja wa madaktari waliojiuzulu.

Wagomaji hao wamebaini kwamba wanafanya kazi katika mazingira magumu, huku mshahara ukiwa ni mdogo mno.

Mwezi Novemba 2019, Waziri wa Afya Agnès Buzyn alipendekeza nyongezo ya mishahara kwa wafanyakazi wa hospitali za mji wa Paris. Lakini, pendekezo hilo bado ni ndoto kwa madai ya wagomaji.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.