Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Wafanyakazi wasio na ujuzi kupigwa marufuku kuingia Uingereza

Waziri Mkuu Boris Johnson wakati wa mjadala katika Baraza la wawakilishi baada ya hotuba ya Malkia huko London, Desemba 19, 2019.
Waziri Mkuu Boris Johnson wakati wa mjadala katika Baraza la wawakilishi baada ya hotuba ya Malkia huko London, Desemba 19, 2019. UK Parliament/Jessica Taylor

Uingereza itaanzisha mfumo mpya wa uhamiaji baada ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ikitoa kipaumbele kwa wafanyakazi wenye ujuzi duniani kote, imetangaza serikali ya Uingereza, ambayo inatarajia kuachana na kutegemea wafanyakazi wa bei rahisi kutoka Ulaya

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, athari za kuwasili kwa idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Umoja wa Ulaya ni moja wapo ya mambo makubwa ambayo yalipelekea raia wa Uingereza kupiga kura kwa wingi kuunga mkono Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya mwaka 2016.

Serikali imehamasiha waajiri kuacha kutegemea wafanyakazi wa kulipwa mshahara wa chini kutoka Ulaya na kuwekeza zaidi katika kudumisha wafanyakazi na kuendelezea teknolojia.

Serikali ya Uingereza iliwahi kusema katika miaka iliyopita kwamba inataka kupunguza wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Pamoja na mfumo huo mpya wa uhamiaji, viza zitatolewa kwa wahamiaji kulingana na ujuzi wao, kiwango cha elimu, mshahara au taaluma.

Wakati wa mchakato huo mhamiaji atakuwa anapewa alama 50 iwapo atatimiza vigezo hivyo.

Kwa ujumla itakuwa lazima kwa mhamiaji kufikisha alama 70 ili aweze kufanya kazi Uingereza huku pia akipata alama kulingana na kiwango chake cha elimu, mshahara atakao kuwa anapokea na kufanyakazi katika sekta zenye upungufu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.