Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USALAMA

Ujerumani: Wanane wauawa katika mashambulizi ya risasi karibu na Frankfurt

Mwili wa mtu aliyeuawa katika moja ya mashambulizi ya risasi ukilazwa nyuma ya gari hili lililoharibiwa huko Hanau, jioni ya Februari 19, 2020.
Mwili wa mtu aliyeuawa katika moja ya mashambulizi ya risasi ukilazwa nyuma ya gari hili lililoharibiwa huko Hanau, jioni ya Februari 19, 2020. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Maafisa wa usalama nchini Ujerumani, wanaendelea na msako mkubwa, kuwatafuta watu waliotekeleza mashmabulizi mawili ambayo yamesababisha vifo vya watu wanane.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi bayo yametokea katika vilabu viwili vya kuvuta shisha katika eneo la Hanau, karibu Kilomita 20 kutoka mji wa Frankfirt.

Muda mfupi baada ya mashambulizi hayo, polisi wameonekana katika eneo la tukio, huku wengine wakitumia helikopta kuwasaka waliohusika.

Shambulizi la kwanza, lilitokea saa nne usiku siku ya Jumatano, baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwauwa watu watoto katika kilabu ya moja na baadaye kwenda katika eneo lingine na kuwauwa watu watano akiwemo mwanamke mmoja.

Haijafahamika iwapo, mashambulizi hayo yalitekelezwa na mtu mmoja au watu wengi, na lengo la mauaji haya, halijafahamika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.