Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA VIRUS

Ufaransa yapiga marufuku mikusanyiko mikubwa, kujihami na virusi vya Corona

Competitors take the start of the 21st edition of the Paris Half-Marathon on March 3, 2013 in Paris.
Competitors take the start of the 21st edition of the Paris Half-Marathon on March 3, 2013 in Paris. LIONEL BONAVENTURE / AFP

Mbio Marathon zilizokuwa zimepangwa kufanyika Jumapili hii jijini Paris, Ufaransa, ambapo wakimbiaji zaidi ya 44,000 walikuwa wamejisajili kushiriki, zimeahirishwa kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya Corona, waandaaji wa mbio hizo wamethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kusitishwa kwa mbio hizi lilitolewa baada ya Serikali ya Ufaransa kuagiza kusitishwa kwa mikusanyiko ambayo itakuwa na watu zaidi ya 5,000 katika matukio ya ndani nay ale ya viwanjani.

Waziri wa afya wa Ufaransa, Olivier Veran, alisema katazo la matukio ya ndani linaenda sambamba na katazo la matukio ya nje ambapo huenda watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona wanaweza kuambukiza wengine.

Hata hivyo makataa haya hayataathiri mechi za ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1, ambapo mechi kadhaa zinachezwa.

Serikali imesema mechi hizi hazijaahirishwa kutokana na kuwa zinachezwa katika miji ambayo hakuna maambukizi ya virusi vya Corona, tofauti na hali ilivyo jijini Paris, Ufaransa.

Wizara ya afya imesema kuna kesi mpya za watu 16 nchini Ufaransa na kufanya idadi yao kufikia watu 73 walioambukizwa tangu mwanzoni mwa mwezi Januari.

Hadi sasa ni watu wawili pekee wamethibitishwa kupoteza maisha ambapo ni mwalimu mmoja na mtalii mmoja kutoka China.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.