Pata taarifa kuu
UINGEREZA-JOHNSON-CORONA-AFYA

Coronavirus: Boris Johnson aingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Hospitali ya St. Thomas huko London ambapo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye anaugua ugonjwa wa Covid-19, alilazwa Jumatatu Aprili 6.
Hospitali ya St. Thomas huko London ambapo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye anaugua ugonjwa wa Covid-19, alilazwa Jumatatu Aprili 6. REUTERS/Henry Nicholls

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameendelea kuhudumiwa usiku kucha katika hospitali inayopatikana katikati mwa mji mkuu London baada ya hali yake ya afya kuwa mbaya.

Matangazo ya kibiashara

Boris Johnson alipatikana na virusi vya Corona siku kumi na moja zilizopita lakini bado anaendelea kusumbuliwa na kikohozi cha kuendelea na homa kali.

Taarifa rasmi ilibadilika ghafla Jumatatu jioni. Baada ya kujaribu kupuuzia hali hiyo, ofisi ya Waziri Mkuu ilitangaza Jumatatu jioni kwamba hali yake ya afya imezidi kuwa mbaya, mwandishi wetu huko London, Muriel Delcroix, amebaini.

"Baada ya adhuhuri, hali ya afya ya waziri mkuu ilizidi kudhoofika na kwa ushauri wa timu yake ya matibabu, alihamishiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali anakolazwa," alisema msemaji wa ofisi ya waziri mkuu Jumatatu jioni.

Ofisi ya waziri mkuu (Downing Street) ililazimika kukubali kwamba Boris Johnson alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi cha hospitali kuu ya St. Thomas karibu saa 7:00 usiku, alipokuwa na tatizo la kupumua.

Kwa sasa nafasi ya Boris Johnson inakaimiwa na waziri wa Mambo ya nje Dominic Raab.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.