Pata taarifa kuu
UINGEREZA-JOHNSON-CORONA-AFYA

Coronavirus: Uingereza kuanza kulegeza vizuizi vya kupambana na Corona

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alikuwa anapatiwa matibabu kwa wiki moja baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alikuwa anapatiwa matibabu kwa wiki moja baada ya kuambukizwa virusi vya Corona. REUTERS/Lisi Niesner

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutangaza hatua kadhaa zinazokuja kulegeza vizuizi vilivyo wekwa kwa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hizo zinatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, baada ya Boris Johnson kurudi Downing Street, na kuendelea na majukumu yake ya kiserikali.

Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa anapatiwa matibabu kwa wiki moja baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Kulingana na Gazeti la Telegraph, Boris Johnson alikuwa na mazungumzo na mawaziri wake kuhusu "marekebisho" yanayotakiwa kufanywa kwa marufuku ya kutembea ili kuwezesha makampuni na shule kufunguliwa tena.

Janga la Covid-19 limesababisha vifo vipya 413 katika masaa 24 katika hospitali mbalimbali nchini Uingereza, na kusababisha jumla ya vifo vya 20,732 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.