Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Zaidi ya kesi 177,000 za maambukizi zathibitishwa Ujerumani

Ujerumani yaandelea kuathirika na virusi vya Corona.
Ujerumani yaandelea kuathirika na virusi vya Corona. Ina FASSBENDER / AFP

Idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zilizothibitishwa nchini Ujerumani imeongezeka hadi 178,000, baada ya visa vipya 513 kuripotiwa siku moja iliyopita, Chuo Kikuu cha Robert Koch (RKI) kimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chanzo hicho, vifo zaidi ya 83 vimerekodiwa ndani ya saa ishirini na nne zilizopita, kwa jumla ya vifo 8,193 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ujerumani ilifikia hatua mpya mapema mwezi huu ya kuanza kulegeza vizuizi ikiwa ni pamoja na kufungua tena majumba ya makumbusho na sehemu za ibada na viwanda kadhaa vya magari, lakini wanasiasa wamegawanyika kuhusu hatua hiyo.

Mapema Wiki hii Mkurugenzi mkuu wa WHO, Dr. Tedros Adhanom Gebreyuses alisema mapambano ya janga hilo ni lazima yapewe kipaumbele, ingawa maradhi ya Covid-19 yanaendelea kusababisha vifo na kudhoofisha uchumi kote ulimwenguni.

Hayo yanajiri wakati rais wa Marekani Donald Trump amelituhumu shirika la Afya Duniani, WHO, kuwa ni kibaraka wa China na limeshindwa kufanya vya kutosha kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Kauli hiyo ya Trump inakuja siku moja kabla ya kutishia kuondoa moja kwa moja ufadhili wa Marekani kwenye shirika la WHO.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.