Pata taarifa kuu
NIGERIA-UISLAMU

Shirika latetea kuvaa Hijabu shuleni Nigeria

Viongozi wa shule katika Jimbo la Lagos wameomba walimu kutopiga marufuku au kuamuru wanafunzi kuondoa Hijabu zao shuleni
Viongozi wa shule katika Jimbo la Lagos wameomba walimu kutopiga marufuku au kuamuru wanafunzi kuondoa Hijabu zao shuleni REUTERS/Goran Tomasevic

Shirika la Kiislamu nchini Nigeria limeonya dhidi ya marufu ya kutovaa Hijabu katika shule mbalimbali za umma katika Jimbo la Lagos. Jumuiya ya Kiislamu ya Nigeria imetoa onyo hilo Jumatatu hii, siku ya kwanza ya mwaka mpya wa shule, kufuatia uamuzi wa mahakama mwezi Julai dhidi ya kupiga marufuku mwanafunzi yeyotekuvaa Hijabu katika Jimbo la Lagos

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rufaa katika jimbo la Lagos ilitoa uamuzi unaoruhusu kuvaa Hijabu katika shule za msingi na sekondari katika Laagos, kusini-magharibi mwa Nigeria.

Kupiga marufuku kwa mwanafunzi au kuwaadhibu kwa sababu ya kuvaa Hijabu ni katika hali ya "kuwanyanyapaa" ameonya Saheed Ashafa, kiongozi wa jamii ya Waislamu nchini Nigeria.

"Hata kama hatutarajii kwamba mwalimu anaweza kupiga marufuku mwanafunzi kuvaa Hijabu, tunawaomba wanachama wetu kuhakikisha kuwa wasichana wanakataa kuondoaHijabu zao," ameongeza kiongozi huyo, akinukuliwa katika vyombo vya habari vya Nigeria.

chama cha viongozi wa shule katika Jimbo la Lagos kimeomba wanachama wake kutopiga marufuku au kuamuru wanafunzi kuondoa Hijabu zao shuleni, kwa mujibu gazeti la Nigeria la Vanguard.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.