BURKINA FASO

Machafuko mapya mjini Koudougou nchini Burkinafaso

Gari zilizo teketezwa kwa moto mjini Koudougou April  2011.
Gari zilizo teketezwa kwa moto mjini Koudougou April 2011. AFP

Machafuko mapya yamezuka nchini Burukina Faso katika mji wa Koudougou ambao wauzaji wa maduka wenye hasira pamoja na wanafunzi wameichoma moto nyumba ya meya pamoja na kituo cha polisi.

Matangazo ya kibiashara

Machafuko haya mapya yanakuja kutokana na wauzaji hao wa maduka kuchukizwa na hatuwa na meya Seydou Zagre na viongoizi wa chama tawala kutangaza kuyafunga maduka zaidi ya arobaini ambayo yameshindwa kulipa kodi.

wamiliki hao wa maduka wakashikwa na hasira kutokana na amri hioyo kitu ambacho kikawapa upenyo wanafunzi hao kuingia kwenye mkumbo huo na kufanya ghasia zilizoambatana na kuchoma moto kituo kikuu cha polisi katika mji huo.

mashuhuda wa tukio hilo wamesema wamiliki hao wa maduka wakiwa na hasira walifaanikiwa kuchoma moto pia nyumba ya Meya Zagre pamoja na baadhi ya ofisi za Umma za Maendeleo ambazo zimeanzishwa.

ghasia hizo zinatajwa kuwa ni muendelezo wa ghasoia ambazo zilizuka baada ya wanajeshi kutaka kufanya mapinduzi ya kutaka kuiangusha serikal ya rais Blaise Comapaore wakidai nyongezo ya marupurupu.

wachambuzi wa mwaswal ya kisiasa wanaona kuwa kile kinacho tokea kwa sasa nchini Burkina Faso kinaweza kulets uvujaji mkubwa wa damu iwapo hali hiyo haitadhibitiwa mapema kutokana na makundi mbalimbali kujumuika kwenye ghasia na mchafuko yanayotokea.