Libya

Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji nchini Libya

milipuko ya April 14.2011.
milipuko ya April 14.2011.

Kundi la maafisa kutoka Umoja wa Mataifa limetumwa mjini Tripoli kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya. 

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuteuliwa na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa jopo hili linatarajiwa kuwasili mjini Tripoli kuchunguza mauaji yaliotokea punde tu utawala wa Libya ulipoanza kushambulia waandamanaji wanaompinga kanali Muammar Gaddafi.
 

Serikali ya Libya kupitia msemaji wake, Musa Ibrahim, imesema itashirikiana kikamilifu na jopo hilo la wachunguzi ambalo pia litachunguza madai ya mauaji yaliotekelezwa na waasi na majeshi ya Nato.

Kuna taarifa kuwa tangu maandamano ya kumpinga Kanali Gaddafi yaanze watu wamekimbia makazi yao, wengine wameteswa na hata kuuawa.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
 

watu waliojeruhiwa wamekuwa wakisafirishwa na meli  hadi mjini Benghazi kupata huduma za matibabu.

Mchambuzi wa mwaswala ya haki za binadamu mwanasheria k

utoka kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania anazungumza kuhusu hali ya haki za binadamu inayoendelea huko Libya.