Burundi

Viongozi nchini Burundi wasitisha Kipindi cha radio ya umma RPA

Nembo ya RPA
Nembo ya RPA (RPA)

kipindi kinachopendwa na raia wengi kwenye radio ya umma RPA kimesitishwa na baraza la utangazaji habari CNC nchini Burundi

Matangazo ya kibiashara

Baraza linalo chunguza uandishi habari nchini Burundi CNC, limechukuwa uamuzi wa kusitisha matangazo ya kipindi"Kabizi" (Anaefahamu) kwa muda wa siku 4. Radio hiyo imechukuwa uamuzi wa kusitisha vipindi vyake vyote badala yake hupiga muziki pekee ili kuonyesha kuwa wanapinga vikali hatuwa hiyo ambayo inakuja kuwanyima haki raia.

Kipindi hicho huwapa fursa wananchi kwa muda wa saa nzima kutowa maoni yao kuhusu mambo tofauti, huwapa nafasi pia wanasiasa walioitoroka nchi kuzungumza na kutowa maoni yao kuhusu mustakabali mzima wa nchi yao.

Mkuu wa CNC Pierre Bambasi afasiri kuwa sababu za kusitisha kipindi hicho ni baada ya mwananchi mmoja ambae alijinasibu kuwa mpiganaji zamani kumshumu moja kwa moja kupitia kipindi hicho rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwamba aliwahi kummalizia maisha mtoto mchanga wakati wakiwa maguguni.

Upande wake mkuu wa radio hiyo RPA Eric manirakiza amesema kuwa CNC haina uwezo wa kusitisha kipindi chochote kwenye radio bali ni mkono wa utawala ndio unafanya hivyo. kioongozi huyo amesema wameamua kuendesha huduma za dharura pekee kama kudhihirisha maskitiko yao.